Monday, April 14

Kitimoto toka Moshi

  Raha ya safari, upate wenyeji watakaojitolea muda wao kukuonesha maeneo mbalimbali ya sehemu umetembelea. Nawashukuru sana wenyeji wangu wa Moshi kwa kutenga muda wao na kuwa nami na wenzangu tulioambatana.
  Usiku wakatujuza kuna eneo huchemsha nyama ya nguruwe. Kiukweli kabisa sijawahi kupishana na upishi wa namna hii.  Nilivyojuzwa ni kwamba, mpiko wake ni, unachemsha hii nyama, unaongeza maji na viungo, unaichemsha hadi iweze kuiva kwa kuchemshwa tu. Haiwekwi mafuta, bali viungo kama karoti n.k na inakua tayari kwa kula
Muonekano wake unakuwa hivi...


  Ilisindikizwa na mboga ya majani ya mnafu iliokaangwa na vitunguu

   Pia kulikua na salad kama mboga ya mnafu haujakupendeza

  Kwa pamoja mlo ulionekana hivi

   Hii yote ilipatikana kule kule Moshi, maeneo ya viwanja vya memorial, Tulipopata menu hiyo pajulikana kama Scorpion.

No comments:

Post a Comment