Monday, December 30

Twaenda likizo kidogo nje ya dar iliyo salama

   Baada ya kazi nzito tuliyofanya pamoja kwa mwaka mzima wa 2013, tumetoka kidogo nje ya Dar iliyo salama, kwenda kujipumzisha kidogo, kutoa uchovu na kukaribisha mwaka tukiwa karibu na wanafamilia wetu.
   Safari ilikua nzuri sana, maana tulipita pande zote kasoro matumizi ya reli.
Tulipaa angani, shukrani kwa Precision air kwa kutupa nafasi huku tukiwa tumechelewa, kisha tukaingia kwa basi, tukavuka ziwa kwa kivuko na kukamilisha safari kwa njia ya ardhini ambapo tulipanda basi tena. 
   Hakika safari ilikua ndefu, ila yenye historia nzuri mno, na kwa sala za wanafamilia na Rafiqs waliokua wanajua kuhusu safari yetu, tulifika salama, na tungependa kushare nanyi mandhari ya safari.....
  Tukiwa kivukoni tulipata mandhari ya ziwa

  Na hapa ni barazani mwa nyumba tunayoishi. Nachopenda zaidi ni mandhari tulivu, hakuna jua sana wala joto, mimea inakua kwa raha na utulivu ule wa kupumzika unaohitajika wapatkana hapa

   Kufika tu, fast tukaangalia je kuna nini cha kuchuma na matunda haya ndio tulikutana nayo. Last time tulikua hapa mapema Disemba, tulipata kuchuma maembe toka mtini, twasafisha na kuyala. 
  Safari hii tumekuta kuna mapera na matopetope.
    Hata tuwapo likizo ni ngumu kukaa mbali na mapishi, hivyo tutakuwa tunawajuza yalojiri toka huku.... tumepika na tunakula nini mpaka tutakapo rejea Dar.
   Kwa instraram tufwate @menutimes. Kwa facebook page yetu ni www.facebook.com/MenuTime na kwa twitter ni @menutimetz.

No comments:

Post a Comment