Friday, June 28

Wazijua shikilimu za Nelwa's Gelato weye......

    Nawaleta kwenu kina Nelwa's Gelato Enterprises, kampuni ya mwanadada Mercy Kitomary, ambae anatengeneza Ice cream kwa mkono wake mwenyewe. 
   Usijiulize ameanza lini, we jua yuko vyema na product anayotoa imesimama, yaani inaweza kulika kwa kila mmoja wetu katika rika tofauti. Yuko vizuri na amejipanga. 
    Hiyo ndio logo yake, na amenihabarisha ati anafanya hadi delivery 
   Anafanya kazi yake kwenye matamasha mbalimbali kama Nyama choma festival iliyopita alikuwepo, kwenye private parties kama sherehe za kuzaliwa n.k, na sasa hivi ana banda lake kule Sabasaba kwenye maonesho.  
 Sasa akiwa mzigoni, popote pale shangwe ilipo na ice cream inapohitajika, huja kwa muonekano kama huo apo chini, akiwa kikazi zaidi, yeye na timu yake yote. Cheze Nelwa's Gelato weye......
  
       Nikuhabarishe baadhi ya ladha za ice cream zinazotengenezwa nao ni pamoja na flavours cookies cream, coconut peanut butter, strawberry, froyo, vanilla na nyinginezo nyingi, mtafute kupitia 0754 938 577 kisha sema nae ladha ile unataka. 
    Wikiendi ndo hii inaanza, tushakujuza nini cha kujifurahisha nacho iwapo upo home au popote ambapo utaweza kufikiwa na Nelwa's Gelato Enterprises. 
    Kutoka Menu Time, tunawatakia mapumziko mema Rafiqs. Kuna lolote..... share nasi kupitia menutimes@gmail.com


No comments:

Post a Comment