Siku ilianza vyema, ka-jua kwa mbali na mambo mengine mazuri, kisha mida ya mchana ka-mvua kakaamua kutudondoshea baraka na kutuongezea neema na amani, na baada ya hapo, shughuli ikaendelea vyema salama salimini.
Nisiwachoshe sana, nataka muone kwa picha na leo tunaanza na hizi chache.... karibuni!!Rafiqs walianza kuingia mida ya saa nne na nusu, na wengi walipata taarifa toka facebook pages za Menu time na K.A.B.L.E, twitter pamoja na radio
Ilikua ni muda wa kufurahi tu, toka waingia mpaka watoka, kwani kulikua hamna shida wala karaha
Kakaz, dadaz, ankoz, antiz, baba, mama na wengineo walijumuika kuleta watoto wapate kuwa moja ya sehemu ya mabadiliko. Hakika siku ilifana!!
Tulipata jumla ya watoto zaidi ya 45 waliofika kuja kuwa sehemu ya mabadiliko wakiungana na wale wa kutokea Malaika Orphanage Foundation ya Kinondoni
Rafiq walijitolea katika kulipia baadhi ya mambo wakiwa palepale Mbalamwezi Beach Club na kwahilo tunasema asanteni sana na tunawaomba muendelee na moyo huo huo jamani, kwani waswahili twasemaaaa kutoa ni moyo ......
Hakika ilikua ni siku ya kujuana na kubadilishana mawazo, kucheka, kufurahia na kadhalika!!
Tunaendelea kuwajuza mengine mengi kwa mpango wa picha kwani hatuwezi sema sana na kwa ufasaha zaidi ya picha zinavyojieleza.
No comments:
Post a Comment