Menu yao kuu ni vyakula vya majini a.k.a sea food na naamini ndio maana wakaita jina la Samaki Samaki. Na mara zote napokula kwao, huwa nafurahi maana vyakula vyote ni fresh muno.
Moja ya menu ya samaki samaki ni hii hapa, ambapo kuna viazi, samaki wa baharini na salad pembeni. Kisha kwa ubunifu vikorombwezo vinawekwa kwenye sea shells, ambapo kuna tomato, mayonnaise, pilipili na hii ya kijani sikupata jina lake ila ni tamu muno, ina mchanganyiko wa kitunguu swaumu flani na vinginevyo.
Kuonesha umahiri na ujuzi wao, siku ya Nyama choma, ile shughuli iliyofanyika pale Postal ground, wakiwa ndani ya banda zuri, walibadili jina na kuitwa Masai masai na kwa hilo walionesha umahiri wao katika uchomaji nyama. Nakuonesha mishkaki jinsi inavyoonekana ikiwa jikoni, yaani bado yaendelea kuiva.
Fanya hivi, kuniamini vyema nachoongea, nenda kawatembelee. Kwa Samaki samaki iliyopo pale Mlimani city siku ya Jumatatu yaitwa Mashujaa day na siku ya leo Jumatano ni usiku wa kupigwa nyimbo za zamani, naongelea miaka ileee tukiwa bado wadogo au vijana.
Tukutane pale maana mie lazima niwepo pale Jumatano nikipata sea food huku nasikiliza oldies laini!!
Kutoka kitaani, Samaki Samaki, MT twakujuza
No comments:
Post a Comment