Wednesday, November 7

Menyu ya Dodoma yalipo makao makuu ya Tanzania

   Kutokana na kuwa na marafiqs wengi toka pande tofauti za dunia, naongelea nje na ndani ya Dar iliyo salama, pamoja na nje na ndani ya Tanzania, pia tukavuka boda hadi Uganda na Kenya, tunaweza acha Afrika Mashariki, twende hadi ndani na nje ya Afrika kwa ujumla.
   Kutoka Dodoma, makao makuu ya Dar iliyo salama, Rafiq wa MT alikua ziarani, akifanya utalii wa ndani na mambo mengine binafsi. Katika pita pita zake, aliona ni vyema akiwa anapata mlo wake ashare nasi ili tuweze kuwajuza yaliyomo Dodoma

 
  Yaliyomo kwenye sahani ni ugali, matembele na nyama yenye vipande vya uyoga a.k.a mashroom. Pia kuna kajikachumbari kwa mbali amabcho kinachombeza mlo mzima.
  Robert wa Mlay asante sana kwa kututumia picha hii.

No comments:

Post a Comment