Thursday, September 13

Picha toka kwa Rafiq

   Nimeona na kuonja supu kadhaa, naongelea ya mbuzi, ya ng'ombe,ya  kuku, ya mbogamboga, ya samaki na nyinginezo. Halafu kuna zile za kutoka kwenye pakiti yaani katika mfumo wa unga, unachanganya na maji moto, nyingine unapika kabisa kisha wapata supu yako.
   Ukienda mahotelini au kwenye migahawa ndo utapata za kila aina, yaani wewe na uchaguzi toka kwa menu utakayoisoma.
    George wa T.bonaz katuletea picha ya supu alikua anaipata siku za nyuma kidogo.


Hakusema ameipata wapi au ameipikaje! ila, tutamuuliza atujuze maana naamini wengi tungependa kuionja ladha yake na kuipika vyema pale tutakapopata maelekezo yake.
  George asante sana kwa kushare nasi picha hii. menutimes@gmail.com na menutimetz@gmail.com ndio anwani zetu iwapo wataka kutuletea na kushare nasi picha za menu zako. Karibu!!

No comments:

Post a Comment