Friday, February 24

Zanzibar Pizza

   Moja ya chakula nilionja nilipokuwa Zanzibar na timu nzima ya Menu Time ni zanzibar pizza. hapo unapata zenye ladha tofautitofauti, naongelea ladha ya mbogamboga, kuna ya mayai, ya nyama, ya matunda, ya chocolate na ndizi, yaani ziko aina nyingi, uchaguzi ni wako wewe wapenda ladha ipi.
   Nilichagua ya chocolate and banana, yaani chokoleti na ndizi. Baada ya uchaguzi nilimuomba mpishi/ muuzaji nipige picha kufuatilia hatua anazopitia toka mwanzo hadi mwisho, na kwa ukarimu akaniruhusu. Hii niliomba kwa makusudi ili nije kushare nanyi kwa niaba ya timu nzima ya MT.
  
Kwanza anakua amesonga unga wa ngano katika vipande vidogo vidogo, kisha anachukua kimoja na kukisukuma. Kisha anaongeza kipande kingine juu yake kama hivi:

Kisha anapaka chocolate juu yake, anaweka ujazo wa kutosha haswaa...

Kisha yachukuliwa ndizi inamenywa kwa hatua kulingana na kiasi atakachotumia kwa pizza moja. ndizi almaarufu kwa jina la mkono wa tembo, yapatikana Zanzibar...

Na hivi ndo pizza inaonekana baada ya kukatwakatwa na kuwekwa juu ya pizza tayari kwa mapishi...

 Kwenye kikaangio kilichopo motoni, anaweka siagi kidogo ili pizza isije kugandana na kikaangio, kisha anachukua ile kipande ya chini ya pizza na kuikunja lakini haifuniki kote kama inavoonesha kwenye picha, kisha inawekwa jikoni kwenye kikaango tayari kwa kuivishwa...

Baaya ya dakika kadhaa kuiva upande wa chini, inageuzwa upande wa juu ili iweze kuiva napo, kisha baada ya muda inakua tayari kwa kuepuliwa, na kuliwa.
Ukipenda kwenye sahani waweza kuongezea syrup yenye ladha ya chocolate kwa ladha zaidi

 Nakuonesha tu jinsi wanavyopika, naamini inaweza kupikwa hata majumbani, ila kutoka kwa wataalamu wetu tuliweza pata picha tu na maelezo kidogo, maana mpishi/ muuzaji alikua na wateja wengi wamemzunguka. naamini tukirejea Zanzibar tutatafuta khabari vyema ili kuwajuza nanyi mjaribu majumbani na popote.
  MenuTime inawatakieni mapumziko mema ya wikiendi nyie na familia zenu popote mlipo.

No comments:

Post a Comment