Thursday, February 23

Tukiaga visiwa vya Zanzibar

     Baada ya kumaliza kufurahia Sauti za Busara, siku iliyofuata tukazunguka Zanzibar. Kutokana na sifa zake kwamba ni kisiwa chenye marashi ya karafuu tukaona ni vyema tuende kuangalia mashamba yanayolima viungo mbalimbali vinavyotumika katika kutengenezea mlo mbalimbali.

      Karibuni tuzunguke Zanzibar
                           

   Zanzibar kuna mashamba yaliyotengenezwa vyema na watalii huenda huko kuangalia, lakini kabla ya kufika huko, kuna mashamba ya wenyeji wa Zanzibar ambao hulima na kuuza viungo kwa ajili ya kujikimu mahitaji yao ya kila siku.

  Shamba tulilotembelea lipo barabarani tu, ambapo mwenye shamba ndio alituongoza na kutupa historia kidogo kuhusiana na mazao ya viungo hivyo, na hapa tunawaonesha picha kidogo ili nanyi mfaidi na picha inayoonesha viungo vilimwavyo Zanzibar

Iwapo utatembelea Zanzibar, jitahidi kwenda mashamba haya na kupata historia na pia kujinunulia viungo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Kutoka visiwa vya Zanzibar,
Menu time team inawaaga.

No comments:

Post a Comment