Ukiondoa kusikiliza muziki, pia kulikua na bidhaa nyingi zinauzwa kama khanga, nguo mbalibali, t-shirt za Sauti za Busara, shanga, vidani na mapambo mbalimbali kwa ajili ya kujiremba.
Uzuri maduka/ mabanda haya yanakua wazi hadi sherehe zinapoisha kwa siku hiyo, yaani saa 6 usiku, ndipo wanapofunga, hivyo upo huru kununua usiku nzima.
Hapa nje ya Mjengo wenyewe unakutana na tangazo hilo:
Kuna watu toka kila kona ya dunia, kuanzia Zanzibar, Tanzania, Africa hadi kwingineko dunia nzima, kulikua na watu toka mataifa mengi tofauti duniani, na wote walikuja kuangalia Sauti za Busara na kufurahia muziki na mengineyo
Jukwaa la Sauti za Busara ambapo limekutanisha sauti, nyimbo, mila na tamaduni mbalimbali za wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Siku ya Jumamosi mojawapo ya burudani zilitokea Tanzania na ndio zilikua zinafunga show ya siku hiyo, ambapo walitoa burudani kwa style ya mchiriku, basi kila aliyekuwepo uwanjani pale alijimwayamwaya na kucheza kwa staha na namna anayojua yeye.
Jipange vyema mwakani usiikose Sauti ya Busara 2013,
Kutoka Sauti za Busara, tunaarifu Timu nzima ya MT (MenuTime)
No comments:
Post a Comment