Nimeona niwajuza namna ya kutengeneza Sandwich, ambayo itakugharimu takribani dakika 20 tu.
Mahitaji:
- Kitunguu maji - 1
- Pilipili hoho - nusu
- Nyanya iliyosagwa - 1
- Maziwa - robo kikombe
- Butter kiasi
- Olive oil - vijiko 3
- Mayai - 4
- Cheese (jibini) iliyosagwa/ ya maji kiasi
- Weka kikaangio jikoni, kisha washa moto, ongeza mafuta acha yachemke, weka vitunguu maji na chumvi kiasi
- Ongeza pilipili hoho, huku unakoroga
- Andaa mayai kwa kuyakoroga kwenye kibakuli pembeni, ongeza na chumvi kidogo sana, kisha changanya kwenye kikaango kilichopo jikoni, koroga kwa kuyavuruga vuruga
- Baada ya hapo ongeza maziwa na jibini katika mchanganyiko wote, endelea kukoroga vyema mpaka mayai yanapoanza kuiva
- Ongeza nyanya iliyosagwa (au nyanya ya kopo), koroga vyema mchanganyiko wako mpaka mayai yameiva vyema
- Epua mayai yako kwani yako tayari
- Chukua vipande vyako vinne vya mikate, uvioke kidogo kwenye toster
- Paaka butter upande mmoja ya mkate (waweza tumia peanut butter pia)
- Weka vipande vya matango kwenye upande mmoja wa mkate
- Weka mchanganyiko wa mayai yaliyoiva vyema
- Ongezea na kipande kimoja cha smoked beef
- Malizia kwa kuweka kipande cha pili cha mkate juu yake
- Kata sandwich yako tayari kwa kuliwa
unaionaje??? tuma maoni yako kupitia menutimes@gmail.com
No comments:
Post a Comment