Tuesday, October 11

Menyu ya Hotelini

Moja ya sehemu huwa napenda kupatembelea nikiwa Dar ni Qbar, hii ipo maeneo ya Oyster-bay pale na ni wazuri wa menyu. Ongelea beef mishkaki, sea food, chips, pork etc etc etc..... yaani u name it, they serve it. Ukiingia upande wa vimimina napo wamekaa njema, Moody amenihakikishia kunitengenezea aina tofauti tofauti hapo Ijumaa halafu ntashare nanyi, ila Rafiqs mnakaribishwa kunijoin, fanya hivi, nipigie halafu tupange.
Sasa katika pitapita zangu nikatua hapo, na ki ukweli ni moja ya sehemu nazoziamini tukiwa tunaongelea vyakula vya baharini a.k.a Sea food . Nasema hivyo kwasababu sijawahi kutana na hitilafu yoyote katika menyu zao.
Kwenye menyu kuna kitu kinaitwa BBQ sea food....


Yaliyomo:
Kuna mchanganyiko wa fillet, kamba, ngisi na wengineo wengi... halafu pembeni ni mash potatoes, hii mash yao ni iliyosagwa vyema, hukutani na mabongebonge kabisaaaa. Mtoto wa miezi 5 anakula anashiba kwa kweli. Kisindikizio hapo pembeni ni salad na mayonnaise.
Nakujuza kama unataka kupata sea food ya uhakika ukiwa Dar, pitia Qbar ni moja ya sehemu ya uhakika wa menyu hii.

No comments:

Post a Comment