Wednesday, September 21

Menyu ya kichinese - Mwanza

Raha ya kusafiri ni kujifunza tamaduni mbalimbali ambazo waweza zipata kwa kuona, kuzisikiza, kuonja na kadhalika. Katika kujaribu kupata kuonja tamaduni ya mapishi ya wachina, zoezi hili lilinikuta nilipokua Mwanza pale nlipoamua kwenda kuwatembelea wenzetu wachina. Sehemu yaitwa Yu Long Chinese restaurant mitaa ya Capri point a.k.a uzunguni.
Binti alinishauri nijaribishe menyu hii


Menyu ilikua tamu haina mfano. Wali uliopikwa na mvuke, Kuku zimepikwa na karanga na sauce flani, wabunifu hawa.
Kilichokwenda wrong: Waliponihudumia chakula, hawakuleta vitambaa vya kujifuta iwapo unachafua mdomo au mikono a.k.a napkins wala tissues. Hii si sahihi kabisa, vitambaa au karatasi laini a.k.a tissues ni lazima viwepo mezani wakati wa mlo. Ni usafi unaohitajika kila mara chakula kinapohudumiwa, hata kama mlaji atanawa mikono.

No comments:

Post a Comment