Tuesday, April 1

Mihogo ya Coco Beach

   Tulipata wasaa wa kupita maeneo ya ufukweni, mjini Dar es salaam, tunaongelea Coco  
beach, ambapo ni maarufu sana kwa upepo mwanana, kuogelea na menu mbalimbali zipikwazo pande hiyo.
  Kunakuwa na mix, mishkaki, mihogo, viazi vilivyokaangwa pamoja na vipande vyembamba vya aidha viazi au mihogo vilivyokaangwa na kutengeneza crisps.
   Sisi tulipata kula crisps, mhogo na kiazi cha kukaanga vikisindikizwa na chachandu, kama picha ioneshavyo hapo chini

   Ukipata wasaa wa kupita Coco beach, je ni menu gani hupenda kuipata?

No comments:

Post a Comment