Monday, February 10

Menu toka Geita... mchana wa leo

Katika safari yetu leo tumefika Geita mjini na kukaa kidogo tukifanya yaliyotuleta na pia kuonja menu yao.
   Cha mchana tukakipata sehemu yaitwa Desire park. Kuna mandhari nzuri sana na hata menu yake ni nzuri
  Menu tuliyopata ni kama hii. Yaliyomo ni pamoja na .....
Kuku rosti

Ugali

Pilipili ya kusindikizia

Samaki alorostiwa kwa rojo la haja

Na kwa harakaharaka, sahani yangu ilionekana hivi.

   Tukawashukuru sana baada ya kushiba na kurejea Mwanza mjini. Kujua kesho twaenda wapi usikose kupita hapa hapa.


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment