Tuesday, April 30

Menyu ya usiku

   Pengine tunafikiria wale wanaotaka kukata weight a.k.a wanadiet,au labda tumeshiba huwezi jua, ila usiku wa leo tunapata menu hiyo hapo chini.
   Kuna kamba a.k.a prawns pamoja na karoti, pembeni kuna jibini. Na kushushia kuna bilauri ya mvinyo mweupe a.k.a white wine.!

Kutoka Bukoba aliko Ankoooo

   Kutoka mkoa wa Kagera, Bukoba alipo Amani wa Lyimo a.k.a Ankoooo, ameshare nasi menyu aliyoipata mchana wa leo.
   Kuna maini a kukaanga, kachumbari na vikorombwezo.
Asante Ankoo!!

Cha leo mchana

  Mchana tulikutana na timu imeagiza chakula toka mgahawa wa kichina, na menu hiyi ilikua ni tambi zilizochanganywa na mbogamboga na kamba....
Yapendeza machoni na hakika ni tamu mdomoni

Kifungu kinywa

   Ni Jumanne nyingine nzuri kabisa, tunaianza siku vyema. Kifungua kinywa chetu ni mayai mvurugiko yenye sausage na jibini, kipande cha mkate pamoja na tunda la ndizi. Kushushia na juisi ya maembe!!

Monday, April 29

Menu ya mwisho Mwanza!!

   Tumefurahi sana kuwepo Mwanza, tumefurahia haswa menu zao pamoja na hali ya hewa.
   Kabla ya kuanza safari, tukaona ni vyema tupashe tumbo joto na supu ya samaki ikisindikizwa na chapati. Karibuni!!

Sunday, April 28

Samaki wa Mwanza

   Kila mkoa una sifa zake kadhaa, tulishawahi ongelea sifa za mkoa wa Mwanza a.k.a Rock city.... unakumbuka kuna samaki pale mjini round about ambapo wengi huenda kupiga picha ya kumbukumbu, well ndo moja wapo ya sifa ya Mwanza kwamba utakula samaki wewe mpaka uchoke mwenyewe.
   Utapata wa mapishi tofauti, naongelea wa kuchoma, kubanika, kukaanga wa mchuzi, wa kuchemsha a.k.a mchemsho wa samaki, yaani chaguo ni la kwako.
  Hapa ni samaki choma!!!

Mwanza siku ya tatu!

    Bado tupo Villa park ila leo menu iko tofauti na samaki, hii ni kukuonesha kuwa ni wajuzi wa menu tofauti ukiacha ya samaki ambayo ndo kubwa.
     Kwenye sahani kuna chipsi, mchuzi wenye pilipili, kachumbari na kuku aliyekaangwa. Nilidhani ni wa kidhungu huyo kuku baada ya kumwonja maana alikua mlaini mno, wakaniambia hapa tunatengeneza wa kienyeji tu.
     Karibu Villa park ya Rock city.........

Saturday, April 27

Menu za Mwanza

    Tupo marafiq wengi tuliokutana muda wa chakula cha mchana pande za Villa park ya Rock city. Ukituuliza kwanini twala hapa mara nyingi, sababu zipo nyingi ikiwemo ukarimu, usikivu, huduma bora, chakula kitamu na mengine mengi. Tunakujuza zaidi kwa kutumia picha kwani utaona vyema.
   Kuna ng'ombe aliyechomwa kwenye foil, na aliyechomwa kawaida, kuna kachumbari, ugali, chipsi pamoja na samaki wa kuchoma.
   Karibu Mwanza Mwanza!!

Friday, April 26

Menu ya kwa Obama

   Kwa hisani ya wabongo waishio Marekani, tumetumiwa picha ya msosi waliokula, walisema wamepika wenyewe nyumbani kwao.
   Hapo kuna wali mweupe, mboga ni firigisi rosti..... looks super yummy!!

Mwanza Mwanza!!!

   Leo tuko pande za Rock city, tumeingia asubuhi hii! na moja ya menu tuliyokutana nayo pande za Villa park ni hii hapo chini. Samaki wa kuchoma na chipsi, vikorombwezo vya pilipili. Tamuje sasa?
Tutaendeea kukujuza menu tutakazokutana nazo.

Thursday, April 25

Siku ya kuzaliwa ya Lulu JM a.k.a Mama Menu Time a.k.a Mama Misosi

   Jana tulimtakia kila la kheri katika kukumbukia siku yake ya kuzaliwa, na tulionesha kifungua kinywa chake siku ya jana. 
   Leo tunaona keki aliyopewa na wafanyakazi wenzie, akaikata akiwa ofisini na kuila na rafiq pamoja na wafanyakazi wenzie. Picha ya keki ni hii
     
    Baada ya kusherekea na wafanyakazi wenzie, mama Menu alikwenda nyumbani kwa mama yake mzazi na kuamua kumsuprise kwa kumpikia moja ya chakula akipendacho mama yake.
    Ushuhuda wa menu hiyo ni huu hapa chini ambapo juu kwenye sinia la kuokea kuna vipande vya viazi, vipande vya samaki vilivyolowekwa viungo, vipande vya vitunguu, karoti pamoja na nyanya. Vyote vikawekwa mchanganyiko wa viungo mbalimbali na kuwekwa ndani ya oven ambapo viliva kwa muda wa dakika 45.
    
        Chini  ni sahani ya LJM, ambapo imewekwa mchanganyiko wa viazi na samaki pamoja na viungo, na pembeni kuna salad iliyochemshwa na kuwekwa kwenye friji kabla ya kupakuliwa.
   Kushushia menu hiyo ilikua ni bilauri ya mvinyo mweupe a.k.a white wine. Hakika waliinjoy wakijumuika na dada wa LJM.
   Kutoka nyumbani kwa mama Lulu, Menu Time inawajuza!!

Wednesday, April 24

Kheri ya Kuzaliwa mwanzilishi wa Menu Time

   Nyota yake ni Taurus, amezaliwa tarehe 24 ya mwezi wa nne miaka kadhaa iliyoita. Ni mwanzilishi na mmiliki wa Menu time blog, na Rafiq wa wengi. 
   Menu yake ya asubuhi aliipata ofisini, akitumia ikombe alichojinunulia kama zawadi ya kufikisha miaka kadhaa. Kikombe kimeelezea mengi kuhusu nyota yake ya Taurus

    
    Timu nzima ya Menu Time inampongeza na kumtakia kila la kheri Miss LJM

Tuesday, April 23

Menu Time yatizima miaka 2 leo!!!

   Zilipita sekunde, dakika, masaa, siku, wiki, miezi na sasa miaka miwili toka kuanzishwa kwa Menu Time Blog. Mwaka ulikua ni 2011, tarehe kama hii ya 23 ya mwezi kama huu wa Nne.
   Baada ya ushauri mwingi kutoka kwa marafiq baada ya kuona jinsi gani tuna mapenzi na chakula, walitushauri kuanzisha blog na leo hii twaseema "Asanteni sana" kwa ushauri wenu!!

   Shukrani zetu za dhati twazipeleka kwa, Mwenyezi Mungu, Familia, partners na Marafiq wote wanaotutumia emails za maswali, ushauri, picha n.k, Marafiq wote wanaotembelea blog yetu kila wapatapo muda , Marafiq wote wanaoitangaza blog yetu kwa rafiqs wengine na marafiq wengine wote. Bila ya nyinyi hakika Menu Time haiwezi simama!!!
  Partners, family, Rafiqs, brothers and sisters tuendelee kuwa pamojah katika kuijenga Menu Time ambayo, mwaka huu inadhamiria kufanya makubwa mengi sana.
  Asanteni nyote..... Happy 2nd Birthday to Menu Time!!

Thursday, April 18

Kutoka mitaa ya Namanga

   Leo,tunaangalia pande za namanga, mbele kidogo baada ya kupita pale wanapopika chipsi pajulikana kwa jina la kwa Edo, hiyo sehemu ipo upande wa kulia. Wanauza chakula kitamu muno, na mara kwa mara huwa naenda nyakati za mchana kupata lunch na marafiq
   Moja ya menyu nliyokula ni wali wa nazi, pembeni kuna kisamvu ambacho kimepikwa kwa ufundi.

   Mboga ilikua ni samaki wa mchuzi na alipikwa kwa tui la nazi. Alikua mtamu munooooo
     
   Kusindikizia kulikua na maharagwe kidogo, ambayo ukiyaweka au kuchanganya na wali, basi raha tupu, huku watupia vipande vya samaki wa mchuzi wa nazi.
  
   Nilichowapendea zaidi ni kwamba, wanasikiliza wateja kwa usikivu mkubwa, wako fasta na bei zao ni zileee za kitanzania kabisa, na unatoka hapo umeshiba mno. 
   Pia wana juisi tamu mno, naongelea ya ukwaju, ubuyu, pasheni iliyochanganywa na parachichi na nyingine nyingi. kama haitoshi, pia kuna soda pamoja na maji safi baridi.
   Twaendelea kukujuza kutoka kitaani, ni sisi Menu Time team

Wednesday, April 17

Makange, nyama choma vya Rose garden

   Wiki hii tupo matembezini sana, jana tulikua Kinondoni, leo tupo Mikocheni pale pajulikanapo sana kwa menu ya makange. Nawaongelea Rose Garden ambapo huwa na menu tamu balaa, ukiondoa services nyingine ambapo huzitoa.
   Upo ugali, iwapo we ni mpenzi sana wa menu hiyo, na kwa kukujali afya yako, basi hukuwekea na mbogamboga kwa pembeni

   Halafu kwa wale wasiopenda nyama nyekundu au niseme wapenda samaki, kuna yule almaarufu kama brenda fasi samaki, ana madikodiko kadhaa na kama wataka pilipili nyingi uwataaarifu mapema waweze kukorofisha vilivyo.

   Sasa kwenye makange, kuna ya kila aina. Nianzie na haya ya maini ya ng'ombe.... utapenda kuyala na nini hiyo ni juu yako, ila mboga ndiyo hiyo.

   Afu kuna ile makange ya kuku, ambapo  ni chaguo lako pia wataka kuila na nini. kipimo kinaanzia nusu kuku na kuendelea.

   Na mwisho wa makange katika menu hii ni ile ya firigisi.... ndio kuna ya firigisi kama ulikua hujui na yapatikana hapo Rose garden. nenda kaijaribishe!!

   Mbuzi choma ni moja ya nyama choma inayopatikana hapo, na hii ilikua tayari kwa kuondoka a.k.a take away ambapo inafungwa na vikorombezo vyake, kila ndimu, pilipili na chumvi, ili huko unapofika usipate shida
   Watembelee wapo garden road, baada ya sayansi kama watokea barabara ya chini. Panajulikana kama Rose garden almaarufu kwa makange. Wanapika kuanzia cha asubuhi, kina supu na wengineo, cha mchana na usiku, na hata vile vya kubite mida yeyote sio lazma iwe mlo kamili.
   Tupo pande za mikocheni leo, twawahadithia vya huku!!

Tuesday, April 16

Menyu a.k.a Menu za Kibo Business a.k.a Mbuzini

   Mitaa ya Kinondoni hapa Dar iliyo salama ndipo wanapopatikana hawa mashujaa wa kupika foil. Naongelea foil ya mbuzi na ya ng'ombe ambapo unaikuta tayari ishawiva, wanakuja nayo mezani kwako na kuikata mbele yako, na unawekewa kwa sahani tayari kwa kula. 
   Kusindikizia nyama hiyo, waweza kula na ugali, chipsi, wali au ndizi, na pengine waweza kuila vivyo hivyo. Labda nikudokeze bei tu, kuna ya shilingi 6,000/= na 9,000/= na kuendelea kutokana na mapenzi yako.
   Nsikuchoshe sana pata kuona mambo matamu waliyonayo.... huo ni ugali, kwa wapenda ugali
 

   Sasa kama wapenda salad au kachumbari, mpango mzima ndio huo...

   Na wale wapenda chipsi kila mara, hapa kuna zile nyembamba, tamu afu hazina kulowea mafuta, yaani kavuu

   Walijua kuna wasiopenda nyama nyekundu, hivyo mambo ya kuku wa kuchoma wakahakikisha wamejitayarisha vyema.

   Sasa hii ndo foil ya ng'ombe ambayo tayari ipo kwa sahani tayari kwa kuliwa.... wataka nini sasa??
   Hawa ndi kina Kibo Business, na uzuri nkuibie siri wanafanya kupika kwa ajili ya masherehe ya harusi, kipaimara n.k yaani pale penye mkusanyiko wa watu kwa nia ya kufurahi huku wakila nyama tamu. Wafuate uzungumze nao!!
   Kutoka Kinondoni, sie MT tunaarifu!!!

Monday, April 15

Ugali toka London

   Kutoka kwa Rafiq aishie London, ajulikanaye kwa jina la Ney Fransis, ameshare nasi menu aliyoipika wiki iliyopita akiwa kwake.
   Tusiseme sana, bali tuona kwa picha hii hapo chini

   Kwenye sahani yake, kuna ugali, mchicha kidogo, kachumbari ya vitunguu na nyanya na kandimu kidogo, pia nyama iliyokaangwa akishushia na bilauri ya maji kwa pembeni.
   Kushare nasi ulichokula tafadhali tutumie kupitia menutimes@gmail.com au info@menutimetz.com. Karibuni sana na tunawatakia wiki njema yenye mafanikio Rafiqs

Sunday, April 14

Ya mwisho kuhusu Toto day ya kwanza ya 23.03.2013

   Kitu kimoja tulishauriana na partner wetu bwana Mutta wa K.A.B.L.E Inc ni kwamba tuwe na kumbukumbu ya shughuli hii  zaidi ya picha. Na akaja na wazo la kutengeneza chaa za viganja vya mikono yetu ambapo watoto walilowanisha viganja vya mikono yao na kuweka stamp kwenye kitambaa cheupe ambacho kitatumika kama kumbukumbu ya siku hiyo.
   Rafiqs wakiwa tayari kuweka alama ya kiganja

Toto akisaidiwa na mamii kuweka alama ya kiganja

LJM wa Menu Time, akimsaidia mchina kuweka nembo kwenye kitambaa cha ukumbusho

Baada ya hapo, LJM akaweka alama ya kiganja kwenye kitambaa cha ukumbusho

Muonekano wa kitambaa cha ukumbushoulikua hivi
   Watayarishaji wa Toto day ni K.A.B.L.E na Menu Time wakiwawakilishwa na Mutta na LJM

   Tunashukuru Mungu vyote vilienda sawa, na mida ya jioni tulinyoosha mikono ya shukrani na pumzi ndefu. It was time to exhale!!!
  Kutoka Mbalamwezi Beach Club iliyopo Kawe, naripoti tukio la Toto Day, ni LJM wa Menu Time!! Asanteni kwa kuwa nasi na kutembelea www.menutime.blogspot.com

Saturday, April 13

Tunamalizia yaliyojiri 23.03.2013

   Tunamalizia kukujuza yale yaliyotokea siku ya Toto day, na labda tuseme mapema kuwa, kuna nyingine itakuja hapo mbeleni, kwani tumeona ni jambo zuri na shughuli nzuri ya watoto kukutana na pia shughuli hii ina nia nzuri na manufaa kwa watoto yatima.
   Tumalizie na picha zilizobaki zinazojieleza vyema
Kutoka Sayona tulikunywa juisi na soda za kutosha, na baada ya menu tulishushia na maji yao, Shukrani za dhati kwao Sayona kwa kutusababishia upande wa vimiminika

   Achick investment nae alifika on time na popcorn za ladha ya chumvi na caramel, yaani zilitafunwa kwa raha zetu na zilizobaki Malaika Orphanage Foundation kids walibeba maana ilikua ni siku yao, Asante sana Akuku wa Achick Investment

   Muda wa chakula ulipofika Mbalamwezi Beach Club ndio waliandaa mpango mzima na kwa wageni kama tulivyotangaza, sahani iliuzwa shilingi 10,000/- tu za kitanzania ambapo kulikua na wali wa veggies, chipsi kiasi, kipande cha kuku, sausage pamoja na salad, na unapata juisi au soda ya Sayona kwa gharama hiyo hiyo. Asanteni sana Mbalamwezi Beach Club.

   Tuliuza sahani za kutosha kwa Rafiqs waliokuja kutoa support siku hiyo, na kwa wote walioweza kuhudhuria tunawashukuru sana, na tukutane Toto day ingine inayokuja soon soon!!

   Kutoka Malaika Orphanage Foundation, watoto wakifurahia menu...... kabla hatujaendelea na michezo mingine mingi tu

   Dada Hakika akiwa busy kuwaserve watoto na kuhakikisha wote wamepata mlo wa mchana, Hawaa pia alisaidia zoezi hili na wengineo, Asanteni nyote

  Tulisema menu itakuwepo na tulikula vya kutosha. Tunaamini kwa umoja na ushirikiano tuliopata kutoka Sayona, Achick investment pamoja na Mbalamwezi Beach club, tuliweza kuhakikisha watoto wote wamepata kufurahi siku hiyo kadri ya uwezo wetu tulioweza. Iwapo kuna lolote lilienda kinyume na ilivyotegemewa, tunaomba radhi kwani sote ni binadamnu na tutayabadilisha kwa kuboresha zaidi!!