Wiki hii tupo matembezini sana, jana tulikua Kinondoni, leo tupo Mikocheni pale pajulikanapo sana kwa menu ya makange. Nawaongelea Rose Garden ambapo huwa na menu tamu balaa, ukiondoa services nyingine ambapo huzitoa.
Upo ugali, iwapo we ni mpenzi sana wa menu hiyo, na kwa kukujali afya yako, basi hukuwekea na mbogamboga kwa pembeni
Halafu kwa wale wasiopenda nyama nyekundu au niseme wapenda samaki, kuna yule almaarufu kama brenda fasi samaki, ana madikodiko kadhaa na kama wataka pilipili nyingi uwataaarifu mapema waweze kukorofisha vilivyo.
Sasa kwenye makange, kuna ya kila aina. Nianzie na haya ya maini ya ng'ombe.... utapenda kuyala na nini hiyo ni juu yako, ila mboga ndiyo hiyo.
Afu kuna ile makange ya kuku, ambapo ni chaguo lako pia wataka kuila na nini. kipimo kinaanzia nusu kuku na kuendelea.
Na mwisho wa makange katika menu hii ni ile ya firigisi.... ndio kuna ya firigisi kama ulikua hujui na yapatikana hapo Rose garden. nenda kaijaribishe!!
Mbuzi choma ni moja ya nyama choma inayopatikana hapo, na hii ilikua tayari kwa kuondoka a.k.a take away ambapo inafungwa na vikorombezo vyake, kila ndimu, pilipili na chumvi, ili huko unapofika usipate shida
Watembelee wapo garden road, baada ya sayansi kama watokea barabara ya chini. Panajulikana kama Rose garden almaarufu kwa makange. Wanapika kuanzia cha asubuhi, kina supu na wengineo, cha mchana na usiku, na hata vile vya kubite mida yeyote sio lazma iwe mlo kamili.
Tupo pande za mikocheni leo, twawahadithia vya huku!!
No comments:
Post a Comment