Siku ya Jumapili, tukiwa tumepumzika nyumbani tukaamua kwenda jikoni na kujipikilisha ili familia ifurahie mapishi yetu, wiki days si tupo makazini.
Mara nyingi nikiingia jikoni huwa sipangi nini cha kupika, yaani chochote nachokipika ni baada ya kukikuta humo ndani ya jiko. Na nikiamua kupika ndo kama vile nakua najaribisha mapishi mapya maana wanasema ni vyema kujifunza kila siku, nami napenda kujifunza.
Nilichopika ni kifuatacho:
Ndizi mzuzu za kukaanga, ambapo nilimenya na kuzikaanga kwenye kikaangio chenye mafuta kidogo.
Kisha nilipika mboga mboga ambazo ziliongezewa maembe. Yaani humo ndani kuna vitunguu maji, karoti, pilipili hoho na maembe, vyote vikiwa katika vipande vinavyolingana ukubwa.
Na cha muhimu zaidi ilikua ni vipande vya kuku ambavyo kwanza, nilivimarinate kwa muda wa nusu saa na viungo kama pilipili manga, vinegar, chumvi, curry powder na chicken masala.
Kisha nikaongeza maji kidogo na kuvichemsha kwa nusu saa kabla ya kuviunga kwa pamoja. Ambapo niliongeza vitunguu maji, karoti na pilipili hoho kidogo, blue band na maziwa kwa ladha zaidi na huu ndiyo ushahidi wa pishi hilo
Kwa hiyo jumla menu nliyopika ilionekana hivi katika vyombo tofauti baada ya kuiva.
Na baada ya kupakua, sahani ya LJM ilionekana hivi....
Takribani inakuchukua kama lisaa limoja katika kutengeneza, kutayarisha, kupika na kupakua ,mlo huu, ambapo waweza usindikiza na kimiminika chochote ambacho unapendelea.
Jaribisha kisha tujuze imetokeaje kupitia menutimes@gmail.com
Kutoka jikoni kwa MT, LJM naarifu!!
No comments:
Post a Comment