Tuesday, March 12

Toto day 23.03.2013

   Tunaendelea kuwajuza yanayojiri katika kuitayarisha na kuitengeneza Toto day ambayo inaletwa kwenu na Menu Time pamoja na K.A.B.L.E. Tulisema siku itakua ni Jumamosi ya tarehe 23.03.2013, maeneo ya Mikocheni pale Mbalamwezi Beach.
   Leo tuongelee sababu zilizopelekea kuamua kuifanya Toto day.....
Ntakurejesha nyuma siku ya tarehe 02.02.2013 tulipotembelea kituo cha Malaika Orphanage Foundation kilichopo Kinondoni na kutumia muda wetu na watoto wa pale. Tukaenjoy nao, tulikula, tulicheza na mengineyo mengi.

    
   Wakati tunaaga baada ya kuwashukuru, kuna baadhi ya watoto walikua na ombi lao ifikapo siku ya Pasaka. waliomba kwenda baharini a.k.a beach. 
   Kwa haraka haraka hili ombi ni dogo, lakini tunaongelea watoto 20 pamoja na dada kama 10 hivi, wanaowaangalia kila siku. Peke yetu kama K.A.B.L.E na Menu Time hatuwezi fanikisha vyema zoezi hili bila kuwashirikisha ninyi marafiq zetu, na kutokana na kwamba siku ya Pasaka kuna matamasha mengi na sherehe nyingi ambazo tusingependa zikwaze mahudhurio yenu, tukaona labda tufanye siku chache kabla ya Pasaka. 
   Pia tunaamini kuna Rafiqs wengi wangependa kusaidia kwa namna yeyote vituo kama hiki, ila hawajua njia za kupitia au kufikisha misaada yao, hivyo kwa kupitia siku hiyo, tutajumuika pamoja na kuweza kuwasaidia kwa chochote tulichonacho, ila zaidi kuspend nao muda kucheka nao, kuongea nao, kucheza nao, kuwasikiliza ndoto zao n.k, kwa siku moja kuwafariji wajione wapo sawa na watoto wengine wasioishi kwenye vtuo vya kulelea watoto

      
     Tuna nia ya kutimiza ombi lao, lakini pia tuna nia ya kuwakutanisha watoto wa Malaika na wengine kutoka majumbani kuja kucheza pamoja na kufurahi pamoja kwani wote ni sawa, na mabadiliko yanaanzia tangu udogoni. Tuwajengee wenetu ufahamu huu kuwa wanaweza kuwa sababu ya mabadiliko katika jamii iwapo watashirikishwa vyema.
    Mfanye mwanao kuwa sababu ya mabadiliko. Na kauli mbiu yetu inasema "CHANGE inaanza na MiMi"!!
    Menu Time na K.A.B.L.E inawakaribisha sana sana marafiq wote pamoja na watoto wetu siku hiyo ya Toto day. Tutaendelea kuwajuza mengine zaidi kadri siku zinavyoenda, na Toto day inavyokaribia.

No comments:

Post a Comment