Wednesday, February 27

K.A.B.L.E & Menu Time ndani ya Malaika Orphanage Foundation

 Mwaka huu wa 2013, Menu Time imeangalia mbali zaidi ya menu. Tumeona ni vyema kujishirikisha na shughuli za jamii kadri tutakavyoweza. Tunaamini kidogo tulicho nacho tutaweza kushare na wengine, tutajifunza mengi zaidi ya haya tuyajuayo.
   Tukakutana na ndugu zetu kina Mutta na Hakika ambao ni wamoja wa K.A.B.L.E tukajiunga nao na kuamua kusambaza upendo zaidi kwa watoto waishia katika vituo vya kulelea walio yatima, waliotorokwa na wazazi wao au sababu nyingine iliyowapelekea kuishia hapo.
   Tunaamini pamoja na K.A.B.L.E tuna mengi mno ya kufanya ila kwa kuanza, tulianza na hili......
   Kituo kinajulikana kama Mlaika Orphanage Foundation kilichopo Kinondoni Dar iliyo salama.

   Nia na madhumuni ni kupeleka kidogo tulichokuwa nacho, ambapo kulikua na vyakula, maji ya matunda, nguo, viatu, vitabu na kadhalika, ambapo wenyeji wetu walivipokea kwa mikono miwili na kushukuru sana!





    Tukaingia ukurasa mpya wa kujuana kwa ukaribu kabisa na wenyeji wetu, kwa kuwajua majina, kuongea nao moja, mbili, tatu na kadhalika. Wenyeji wetu ni wakarimu na wacheshi mno.





   Tulikuja kugundua kuwa watoto hawa wana vipaji tofautitofauti walivyozawadiwa na Mwenyezi Mungu, hivyo tukaona kuwa ni vyema tukae pamoja kisha tuone au tuoneshane vipaji vyetu tulivyojaaliwa. Ilikuwa raha sana kushare vipaji. Kuna wanaojua kuimba, kucheza, kurap, kuigiza ilimradi fani mbalimbali



  Tukaendelea na michezo mingine mingi mingi ikiwemo soka. Mpira wa mguu ni mchezo unaopendwa na wengi sana, na haijalishi umri kwamba ni mkubwa au mdogo... tukaona kwanini tusicheze soka la pamoja.... huku wengine wakibembea, wengine wakicheza na maputo na kadhalika.




   Mengine mengi yanafuata kukujuza hali ilimalizikaje katika kituo cha Malaika orphanage foundation.... Endelea kuangalia yaliyojiri

No comments:

Post a Comment