Friday, February 15

Chapati za kihindi a.k.a Naan

   Chakula aina ya chapati sote twakifahamu vyema. Sasa basi kuna aina kibao za chapati. Kuna chapati za maji, kuna chapati nzito, kuna chapati zilizopikwa na tui la nazi, kuna za kuchanganya na matunda, alimradi tu wewe na wageni wako na mapenzi yenu juu ya aina ya upishi wa chapati na vifaa ulivyonavyo katika kukamilisha hilo pishi la chapati muipendayo.
   Moja ya chapati huwa tunapenda kuipata haswa pale tunapotembelea migahawa au mahoteli mbalimbali ni chapati za kihindi a.k.a naan. Hatujajua bado namna ya upishi wake, na tunaamini ipo siku tutadadisi upishi wake, tujifunze na tukishafuzu kidogo tuje kuwamegea nanyi ujuzi ili tuende sawa.
   Moja ya sehemu wanapika pishi hili la naan ni Best bite ambapo unachagua naan yenye ladha uipendayo. Kuna butter naan, garlic naan n.k. Tunayokuonesha ni garlic naan yaani ile iliyowekwa ladha ya vitunguu swaumu. Haswa twapenda ladha ya vitunguu swaumu, na kama ijulikanavyo vitunguu swaumu vina kazi mbalimbali mwilini ukiondoa kuongeza ladha.

    Sasa menu hiyo yaweza kusindikizwa na rosti ya prawns, ng'ombe, maini, maharage au na kimiminika tu, inategemea siku hiyo umeamua kula vipi naan yako. Sisi tulipata na rosti ya kuku a.k.a chicken curry.
   Kutoka Best bite ya Kinondoni, LJM nawajuza!!
Weekend njema tunawatakia, na kuwasiliana nasi ni kupitia menutimes@gmail.com, pia tutafute kwenye face book. Tunaitwa Menu Time

No comments:

Post a Comment