Kila mmoja wetu alisherehekea sikukuu ya Noeli a.k.a Xmas kwa namna ya pekee, ila kuna mambo ambayo hufanana katika usherehekeaji wa siku hiyo. Mambo hayo ni kama kwenda kusali kanisani kwa waumini wa kikristu, na la pili kuandaa mlo maalum kwa wanafamilia, majirani na marafiki, kisha kula, kunywa na kufurahi pamoja.
Wachagga kama ilivyo ada wao huenda Moshi wakisherehekea na familia zao, pamoja na jirani zao wa Arusha. Nimesikia pia makabila mengine kama wanyakyusa, wahaya n.k nao wamekwenda mikoani / vijijini kwao kusherehekea sikukuu hii na familia zao vyema.
Kutoka Hong Kong, kwa daddy Lucian, yeye alisherehekea kwa kupokea ujio wa kaka yake Victor pamoja na mama yao. Na furaha imeongezeka ndani ya familia yake kwani mtoto wake ambaye amezaliwa miezi michache iliyopita alikua anasherehekea sikukuu ya kwanza ya Krismas katika maisha yake.
Picha aliyoshare nasi ni hii ambayo walipika na kula mlo huu siku ya mkesha wa krismas huko Hong kong.
Menu ilikua ni turkey aliyeokwa ambapo alisindikizwa na viazi pamoja na salad (ambavyo havikuoneshwa pichani).
Tunamshukuru sana Lucian, Victor na familia zao huko walipo Hongkong.
Nawe wakaribishwa kushare nasi yale mliofanya na mliyopata kula kipindi cha sikukuu kupitia anwani zetu, nasi tutashare na Rafiqs wote.
No comments:
Post a Comment