Wednesday, August 1

Kifungua kinywa toka jiko la Menu Time

   Mlo wa asubuhi ni muhimu kwa kila mwana wa adamu. Kwa siku nzima kuna rafiqs wanaokula mara 2 tu kwa siku, kuna wanaokula mara 1 aidha iwe mchana au usiku tu, na wengine mara 3 kama ilivyo kwa wengi wetu, na kila mmoja wao ana sababu zake binafsi iwe za kiafya, kifedha, kiimani n.k.
    Kutoka jiko la MenuTime asubuhi ya leo kifungua kinywa chetu kilikua hivi kama hapo chini.Kuna toasted breat, sausage na scramble eggs iliyokarangizwa na nyanya na zabibu kavu. kishushio ni maziwa yaliyochemshwa na milo, na kasukari kwa mbaali kuongeza ladha.

  Karibu tujuze nawe wafunguaje kinywa chako....... tutumia kupitia menutimes@gmail.com au menutimetz@gmail.com nasi tupate kujua.
   Kutoka jikoni asubuhi hii, LJM pamoja na timu nzima ya MenuTime tunawatakia Jumatano njema!!!

No comments:

Post a Comment