Friday, August 3

Chipsi mayai a.k.a zege

   Moja ya menyu inayolika sana au tuseme inayopendwa sana Tanzania ni chipsi mayai ambayo yajulikana sana kama zege. Nielewe vyema hapa sio waweka chipsi peke yake kisha likakaangwa yao na kuwekwa pembeni yake laaa, ni mchanganyiko wa chipsi na mayai kwa pamoja kama linavyochanganywa zege na ndo maana likabatizwa jina na kuitwa zege.
   Wengi twajua kulipika hilo zege ila inategemea unaweka mbwembwe gani wakati wa upishi. Kuna wanaokorogea vitunguu maji ndani ya mayai, wengine huweka pilipili na chumvi humo humo, wengine mpaka nyanya nazo zawekwa, na wengine hata jibini a.k.a cheese, ilimradi kupata ile ladha Rafiq anapenda.
   Mtwara tulipata kuonja zege lao huku likisindikizwa na mboga mbalimbali. Karibuni Ntwara kama wenyeji wake wanavyoliita jina la mkoa wao.
   Ya kwanza ilisindikizwa na kuku wa kienyeji aliyokaangwa. kikorombwezo kilichotumika ni tomato sauce

   Ya pili ilisindikizwa na kamba a.k.a prawns ambao nao wamekaangwa. Kikorombwezo kilichotumika hapa ni kama cha mwanzo, tomato sauce.

   Nina hakika wengi tumeshawahi kupata mlo huu, tujuze zaidi kwa lugha ya picha kwa kukutumia kupitia anwani yetu menutimes@gmail.com au menutimetz@gmail.com . tueleze wapenda kutumia mbwembwe gani katika upishi wa zege
   Wikiendi njema inayoanza leo na mfungo mwema ndo Timu nzima ya MenuTime tunawatakia.

No comments:

Post a Comment