Leo tuangalie ile nyama ya kupikwa kwa moshi a.k.a smoked beef inavyopikwa na ndizi kupitia mapishi ya kichagga. Upishi hili nimefundishwa na mama yangu mzazi. Mama Lulu.
Hapa nilitumia nusu kilo ya smoked beef, ndizi mbili (ila kwenye upande wa aina ya ndizi, waweza chagua iwe mshale au bukoba yaani wewe na mapenzi yako).
Kuniuliza inapatikana wapi hii nyama, ni Peramiho, mkoani Songea. Nilipopata bahati ya kutembelea mkoa wa Songea, Rafiq wetu aitwa Deo aliniagiza mzigo toka kwa mama mdogo. Mama mdogo alinipa zawadi ya kilo moja ya smoked beef.... nilishukuru saana. Za pekee shukrani zimwendee Deo kwa kutujuza kuhusu hii nyama tamu.
Baasi tuanze kupika sasa,
Tayarisha sufuria yako, kisha menya ndizi zako, katakata vipande, zioshe vyema, kisha ziongezee maji safi, chumvi kiasi. Ongeza vipande vyako vya smoked beef ndani ya sufuria hilo. Katakata kitunguu maji kimoja, pilipili hoho moja, nyanya mbili kisha changanya na zile ndizi. weka jikoni, funikia acha viive.
Namna ya kugeuza mapishi haya ni kwa kuyapepeta, ndiooooo, shikilia sufuria lako na vitambaa kuepusha kuungua na kisha pepeta ili mchanganyiko wa juu ushuke chini na wa chini upande juu na viweze kuiva vyema. onja kama vimeiva na kama tayari basi zima jiko epua mlo wako tayari kwa kuliwa.
Mimi wa kwangu ulionekana hivi.....
Jaribisha hii, ila Mama alisema waweza tumia nyama ya kawaida yaani isiyo smoked, na utapata utamu kama huo hapo juu au tofauti kidogo katika ladha.
Tujuze ya kwako inatokeaje baada ya kujaribu kwa kututumia picha yako kupitia barua pepe: menutimes@gmail.com au menutimetz@gmail.com nasi tutashare na wengine.
Kutoka jikoni kwa MenuTime LJM naaga.
Looks delish... Songea kweli noma. We use to have a friend ana ranch, alikiwa mzungu. Alikuwa na kila aina ya nyama. Hata hiyo smoked one.
ReplyDeleteTeamTBonaz huyo mzungu yuko wapi sasa tuweze kupata more nyama
ReplyDelete