Friday, March 9

Menyu ya maulidi

   Jumamosi iliyopita nilialikwa kwenye maulidi ya harusi ya rafiq yangu aitwa Bi Halima. Kama ilivyoada ukiitwa kwenye shughuli shurti ushughulike, ndo maana ya shughuli nzima.
  Kila kitu kilienda sawa, salama salimati, tuliswali na kaswida ziliendelea, ikafuatwa swala ya mchana na mwisho kumzawadia bi Harusi kabla ya kupata maakuli.
  Menu Time inahusika sana hapa kwenye maakuli na kama kawaida Kamera ikafanya kazi yake. karibuni:

  Mpango mzima kwenye meza ulikua hivi, unaona sahani kwa mbaali

Kulikua na biriani ya kutosha, wageni tulipakua mara mbilimbili

Na mchuzi wa kumezea biriani ulopikwa ukapikika. Nyama ya kumwaga na viazi vinakusindikiza
Ndizi zilizopikwa na nyama ya utumbo nazo zilikuwepo shughulini

Mbilimbi ilikuwepo ilotengenezwa na ndimu, nyanya, vitunguu na vinega kwa mbali. Ilikua kali lakini tamu na chumvi kiasi

Sambaru kwa jina lingine Achali ya maembe a.k.a mango pickle ilikuwepo ambayo nilijikuta napakua nyingi utadhani ndo chakula chenyewe

Na sahani ndo ilikua hivi, tusiulize ilirudi kujazwa mara ngapi....

Tujuze unayokutana nayo kwenye misosi, minuso na mitoko unayoalikwa ili nasi tufurahi pamojah, tutumie kupita menutimes@gmail.com

Kutoka Mikocheni LJM wa MenuTime naarifu.

4 comments:

  1. wapi naweza kupata hiyo achali ya maembe please

    ReplyDelete
  2. Waweza kuipata kwenye Supermarket yeyote. Naongelea mango pickle zile za kwenye chupa. Hii ya siku ya maulidi ilipikwa na kina mama flani. Ila ukienda Sinza madukani tafuta zenye nembo ya NIUTU au wapigie kwa namba hii 0713 706 263.

    ReplyDelete
  3. Heheheee, sikuona hiiiiii i loved the lemon chilli it was absolutely delicious

    ReplyDelete