Sunday, February 19

Ikwiriri ....

  Niliongelea kuhusu nazi hapo jana, huku Ikwiriri nilipata kujua bei wanazouza nazi nkashtuka kukuta mmoja inauzwa mpaka shilingi 350/= za kitanzania, ilihali mjini nazi moja inauzwa kuanzia shilingi 500 - 1,000/=. Sasa inafika muda unajiuliza kweli nahitaji ladha ya nazi kwenye chakula?? maana mlo mmoja ili ukolee nazi, naongelea kwenye mboga na wali kama wapika na wali basi utatumia walau nazi moja nzima.
  Tufanye hesabu sasa, kwa wiki ambapo kwa siku kama wala milo miwili unaongelea 2,000/= kwa siku na siku 7 hiyo ni 14,000/= hapo umenunua nazi tu, bado nyanya, vitunguu, chumvi na hiyo mboga yenyewe utakayopika..... kweli maisha yamepanda bei!!
  Basi moja ya menyu tuliyoionja wakati tupo huko ni hii hapa:


   Hapa kuna wali wa nazi, na ndizi za nyama ambazo nazo zimeungwa kwa tui la nazi kuongeza ladha. hakika chakula kilikua kitamu mno, na rahisi mno kupika.
   Tulipata kuelezewa jinsi wao wanavyopika na wakati tunajaribisha kupika upishi wao basi tutawajuza zile hatua za kufuata mpaka mlo huu utokee.
 Najua watu wa Pwani, Bagamoyo,Tanga, Mombasa watakua wamefarajika kidogo kuona mlo kama huu maana ndo mambo yao, wanasema mambo ya pwani.

Bado twaripoti toka Ikwiriri.

No comments:

Post a Comment