Friday, August 12

Macaroni na Nyama ya kusaga na jibini

Baada ya kufurahia matumizi ya jibini kwenye chakula, nimejaribu kutumia tena katika mapishi ya leo. Nimeamua kupika Macaroni na nyama ya kusaga, kisha nikanyunyuzia jibini iliyokwaruzwa, kisha nikaweka mlo wote kwenye oven na kuoka kwa muda kidogo ili kuruhusu ile jibini ichanganyika vyema.

Unakumbuka nilieleza namna ya kupika macaroni na nyama ya kusaga katika post yangu ya Tarehe  1 May 2011, basi fuata hatua zote za upishi.

Tofauti ni kwamba hapa nimetumia tambi zile ndefu na sio zile fupi zenye kujikunja. Ila waweza tumia yeyote kati ya hayo ni vyema tu.

Basi ukimaliza nyama yako itaonekana hivi:

 Na tambi zako zitaonekana hivi:

Sasa basi chukua chombo ambacho waweza tumia kwenye oven. Kisha weka macaroni yako nusu, kisha weka nyama ya kutosha. Mlo wako utaonekana hivi:

Ongeza macaroni yaliyobaki kwenye chombo chako na itaonekana kama hivi:

Tayarisha oven yako kwa kuiwasha tayari kwa kuweka mlo wako pale utakapomaliza kunyunyuzia jibini. Kwaruza jibini yako a.k.a cheese na uitandaze juu ya macaroni ukiwa unahakikisha unaitandaza vyema ienee pande zote, muonekano waweza fanana na huu:
Weka mlo wako katika oven yako uliyokua umeiwasha tayari, na oka kwa muda wa dk 10 katika nyuzi joto 120. Baada ya hapo jibini itakua imeyeyuka na kujichanganya vyema huku nyingine ikiwa imebaki juu. Epua mlo wako tayari kwa kuliwa.

Unaweza changanya na mbogamboga za majani, na salad yako pembani tayari kwa kula. Kwenye upande wa kinywaji inategemea wapenda nini zaidi, ila ukishushia na mvinyo mwekundu a.k.a red wine inashuka vyema zaidi, na kama si mtumizi wa kilevi basi hata juisi yeyote au maji safi yaweza kukamilisha mlo huu.


No comments:

Post a Comment