Friday, January 10

Kifungua kinywa & cha mchana kutoka Shieni

Enhee... tumeamkaje leo... Ijumaa si ndio hii????
Nimepakumbuka kwetu Sinza, Shieni bar ndo yapatikana supu hii..
Ni supu ya kuku wa kienyeji, pembeni ikisindikizwa na chapati

  Na mchana au muda wowote baada ya kufungua kinywa, waweza jipatia zege a.k.a chpsi mayai yenye mbogamboga ndani na mishkaki upendayo kwa pesa ndogo tu za kitanzania

Ukiwa waagiza zege, huwa unapenda lichanganywe na nini zaidi ya mayai na chumvi???
Muwe na wikiendi njema sana!!

No comments:

Post a Comment