Wednesday, June 5

Utumbo ulochanganywa na mchicha

   Mboga hii mara nyingi kama inanoga ukiwa unaila na ugali vileeee, au we unaonaje? 
Yani hapo kuna nyama ya utumbo ilioungwa na mchicha afu ikamaliziwa kuungwa na tui la nazi, basi utamu unakua umefika mahali pake haswaa!!

   Inapatikanika pande kadhaa mjini Dar iliyo salama, ila hii hapo juu tulipishana nayo pande za Mikocheni, Garden Rd pale Rose garden.
   Jitahidi ukapate yako mida ya mchana afu kwa ushauri tuuu pata na ugali, shushia na maji safi ili kukamilisha mlo wako wa mchana.

No comments:

Post a Comment