Kifungua kinywa sio lazima ukipatie nyumbani. Popote pale inawezekana, iwe ofisini, mgahawani, nyumbani au kwengineko,cha msingi muda uwe wa asubuhi na uwe ndo mlo wako wa kwanza,ikimaanisha ndio mlo unaofungua kinywa.
Asubuhi moja nilipita mitaa ya Tabata, nikawakuta Rafiqs wakipata kifungua kinywa chao, ndani ya baa moja matata sana.
Hii ni supu ya utumbo. Chuzi halijaongezwa maji wala kiungo chochote. Pilipili, ndimu na chumvi huwekwa pembeni kwa ajili ya kujiongezea ladha kama utapenda.
Menyu hiyo kwa hela taslim za kitanzania shilingi 2,000/= tu unaipata.
Japokuwa hizi sahani zinasaidia kuweka vitu vingi, na zatumika kwa wingi kwenye mabaa na baadhi ya migahawa binafsi sijawahi kuzipenda kabisa. naona kama kubwa sana!! mtazamo wangu tu!!
No comments:
Post a Comment