Tuesday, June 24

Sea food toka kigambonino

  Bwana Abdallah Gunda katika mihangaiko yake ya hapa na pale nyakati za wikiendi iliyopita, alipatwa na safari ya kwenda Kigamboni almaarufu kwa jina Kigambonino. 
  Akiwa pande zile akaona si haba kujaribu menu zao, ambapo alitua kijiji beach na kuagiza msosi ambao alipendelea.
  Mara kwa mara nikiwa nipo na Abdallah moja ya chakula hupenda ni kile cya majini, yaani kipatikanacho toka kwenye maji,  iwe maziwa, bahari, mito n.k. Hivyo basi uchaguzi alofanya kule nao haukupishana na akipendacho daima ambacho ni sea food.  Karibu kuona lichopata Rafiq toka pande zile

 kwa haraka haraka naoa kuan samaki kwa chini pale, kuna ngisi, kuna kamba wakubwa na salad ya majni kwa chini kusindikizia mlo mzima, huku vipande vya ndimu vimetupiwa kwa juu kuongeza nakshi lakini pia ladha na mwisho kuondosha harufu ya shombo mkononi.
   Ukiwa pande za Kigamboni, iwe waishi huko au waenda salimia, fanya kupita hapo nawe upate sea food yako kama rafiq.
  Asante sana Abdallah wa Gunda, tumefurahi kupokea picha yako.
Kesho tutarejea tena tukiwa naye ila hapa atuonesha menu iliyopikwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment