Wednesday, June 18

Posta, upanga na mambo ya Miksii

  Na kwa kuwakaribisha posta, tulimaanisha pande za Upanga ambapo kuna sehemu wako makini katika upikaji na utengenezaji wa bajia, kababu na miksii ambapo ukianza kwenda hapo hutoacha.
   Muda wa kufunguliwa na mauzo kuanza ni saa kumi na moja jioni pale ambapo wengi tumetoka maofisini, twaelekea makwetu, na huwepo hadi kwenye saa tatu usiku.
  Karibu kuona menu tulizozipata pale tulipowatembelea Rafiqs hawa.
   Tunaanza na miksi ambapo ni mchanganyiko wa mambo mengi matamu na kwa pamoja muonekano wake huwa hivi

  Wengine hawakupenda miksi, bali walitaka wapate bajia au kachori na wanauza sh 2,000 kwa sahani ambapo wasindikizwa na chetna iliyo na kila aina ya utamu, na pilipili kwa pembeni kama utapendelea.

 Kwa ukaribu zaidi na upendeleo
   Tunahama kutoka Upanga, a.k.a Uhindini hadi Kinondoni, na ifikapo kesho ntawajuza yaojiri kinondoni

No comments:

Post a Comment