Thursday, June 19

Kinondoni

   Leo tupo Kinondoni, na ndo mambo ya wikiendi yanaanza na si wote twajua starehe zote zipo Kinondoni, basi mapema tujuzane menu ipi unapata wapi kwa nani  na mengineyo, sababu tunaijua ni kupata utamu
  Sasa pale Hugo Kinondoni wafanya kama wakata kona waelekea palipo baa maarufu sana kinondoni, mkono wako wa kushoto, utaona kontena pale ambapo mambo haya ndo yapatikana. 
Tulipishana na biriana moja matata sana, ambapo ilisindikizwa na tunda la ndizi pamoja na Fanta baridii.

  Kwa pembeni pale alipo Rafiq yetu wa kitambo, bado anafanya mabo yake na ile nyama yetu ilee. Cha leo kilikua cha makange na muonekano wake ni kama huo khapo

  Tunaendalea kujitayarisha na kukutayarisha wewe na wikiendi, na kwa kumalizia tunaenda kuleeeee Masai club mitaa ya Mwananyamala. Hawalali Rafiqs wa pande zile.

No comments:

Post a Comment