Friday, June 20

Masai Club - Mwananyamala

  Ijumaa ndio hii, enhee tujuzane mapemaaaaaa..... leo mtoko wapi, haya kama utabaki nyumbani menu gani watayarisha, na je utakula na nani?
  Wiki iliyotangulia, siku kama ya leo tulipata kufika pande za Mwananyamala, ilipo Masai bar ambapo huko kuna kila aina ya starehe uitakayo. Kuanzia vinywaji, muziki, vyakula na mengineyo.
  Moja ya menu tuliyopishana nayo ni supu ya ng'ombe na ushuhuda ni huo hapo chini. Imesindikizwa na mbogamboga ndani ya supu, kuna ndizi humu na kwa pembeni ndimu na chumvi vya kunogesha mambo

   Kutokana na kwamba sio Rafiqs wote walipendezwa na kupata supu mida ile, basi wao waliamua kuagizia mishkaki, kiukweli ni milaini na mitamu sana sana. Pongezi kwa bwana mpishi.
   Mambo ni mengi yanatokea siku ya leo, karibu kushare nasi yatakayojiri pande ulizopo. Anwani ni menutimes@gmail.com au tufwate kwa social medias... instragram tupo @menutimes na kwenye kitabu sura a.k.a facebook, page yetu ni www.facebook/Menutime.com na kwa twitter ni @menutimetz
  Haya tukutane huko kwa habari zaidi za kiwikiendi.

No comments:

Post a Comment