Tuesday, June 17

Menu za Wikiendi

   Siku ya Jumamosi baada ya kutoka shamba kama ilivyo ada, tukapita pande za Sinza, palipo Shieni bar na kuomba menu ya siku hiyo.
 Tuliletewa kuku wa kienyeji alorostiwa pasi mafuta na kuchanganywa na mchicha, kisha rojo likajitengeneza, na mboga hii ililiwa na ugali.
 

  Naamini kutokana na njaa na hamu ya menu hii, ugali ulisahaulika kupigwa picha, na tunaamini sote twaujua ugali vyema, lakini haimaanishi kwamba ndio utengwe laaaah, mtuwie radhi kwa kutowapa utamu wote.
  Tunaendelea mbele, tukutane kesho tutakapo kujuza menu tuliyopishana nayo mjini Posta.

No comments:

Post a Comment