Monday, June 16

Mambo ya Wikiendi

  Kuna mengi hufanyika mwisho wa wiki a.k.a wikiendi, na katika yote hayo la muhimu ni kusali, kula na kulala katika muda ujipangiao wewe mwenyewe pasi kushurutishwa na mwanaadamu yeyote. 
  Katika wikiendi hii tulipata tembelea maeneo mbalimbali na tutashare nanyi menu zote tulizozipata pale tulipoketi na kuonja utamu waoutengenezao wapishi wa menu hizo.
  Kutoka Nyumani Lounge, mgahawa uliopo karibu na Best bite tulipata menu hii hapa, kuna ndizi na mishkaki. Mishkaki hii ni firigisi,, huku ikisindikizwa na kachumbari na pilipili.
   

  Pia wanatuarifu kuwa siku hizi kuna soseji zile kubwa kubwa, katika upishi uuchaguao wewe mwenyewe na mapenzi yako. Sisi tuliagiza za kukaanga pamoja na vipande vya kuku, na mtazamo wa sahani yetu  ndio ulikua hivyo hapo chini. Kama ilivyo ada, shurti kachumbari na pilipili visindikize menu nzima.
  Tulipata kutembelea sehemu kadha wa kadha na zote tutashare nanyi, kwasababu tunawajali na kuwapenda na tungependa nanyi mkaonje hayo tuliyoyapata. 
Tukutane kesho!!

No comments:

Post a Comment