Wednesday, June 11

Mambo ya TCC Chang'ombe Club

    Katika pitapita zetu jana, tulipata kuwatembelea TCC Chang'ombe Club. Eneo kongwe lijulikanalo na maelfu ya watanzania, na nikiwa pale nilipata kujua kwamba ndio club za kwanza za soka nchini Tanzania, na uwanja ule basi ulipatwa kukanyagwa na wanasoka wengi mno, ambao ni mababu zetu, baba zetu, wajomba na hata kaka zetu, na pengine watoto na wajukuu zetu, inategemea tuliopitia na kuujua uwanja huo muda gani.
   Kitu kimoja kuhusu ule uwanja nachopenda sana ni mazingira yake yako tulivu mno na ni sahihi haswa kwa wale wafanyao mazoezi ya viungo katika kujiweka fiti na maisha.
  Pia upande wetu wa maakuli, wapo vizuri ambapo vyafwatana na muda naamini na matukio pia hutofautiana. Mchana siku za juma kwa ujuzi wangu panapikwa vyakula mbalimbali vya kuungwa, kuchoma, kukaangwa na kadhalika, ni wewe tu na maamuzi yako ya siku hiyo.
  Tusiongee sana, jana menu tuliyopata ni hii hapa,
Samaki wa mchuzi alopikwa na pilipili |(ugonjwa wangu).

   Samaki huyo alisindikizwa na mboga ya maharagwe, mboga ya majani pamoja na wali wa nazi ambao ndo ilikua menu yangu. Pembeni kuna vikorombwezo kama kawaida, huku tukishushia na maji safi ya kunywa.
  Kesho tutarejea kuwajuza menu nyingine zinazopatikana pande za TCC Chang'ombe. Tunawatakia siku njema leo.

No comments:

Post a Comment