Monday, May 5

Mchemsho wa kinyumbani

  Tuanze wiki vizuri huku tukiujenga mwili vyema baada ya mapumziko ya siku hizi mbili. Tunatofautiana na namna tupumzikavyo, ila mwisho wa siku Jumatatu ndiyo hii na shughuli zinaendelea kama kawaida.
   Leo waweza anza siku namna hii, au hata ukaweza kuipata kama menu ya mchana.
NI rahisi maana humu kuna kuku wa kienyeji, viazi vya kuchemsha, karoti, brokoli pamoja na mboga nyinginezo ambazo mwenyewe utapenda kuongezea.
  Kisha wachemsha tayari kwa kuandaa kama mlo


  Wale wasiopenda vyakula vyemye mafuta, au vya kukaangwa, huu ni mlo mzuri sana kwao, pia kwa wale wanaotengeneza miili yao isinenepe bila sababu.
   Tunawatakia wiki njema yenye mafanikio kwenu

No comments:

Post a Comment