Wednesday, June 12

Cha mchana cha leo toka Kinondoni

   Lini mara ya mwisho umepata kula chakula yale mambo ya mboga sita, saba???? au basi hata nne kama sio tatu. yaani namaanisha sio unakula wali maharagwe tu, au ugali kuku basi unashushia na maji na tunda.
   Naongelea kitu cha wali, maharagwe, mchicha kidogo, nyama kidogo na vikorombwezo kadhaa..... inaonekana itakua tamu muno sio, basi ndo menu tuliyokutana nayo mchana wa leo pande za Kinondoni.
   Hapo kuna pilau, maharagwe, mchuzi na kachumbari,,,,,, yote kwa pesa za kitanzania 3,000/- tu.
 
Jinsi tuishivyo Tanzania, ni kwa gharama uichaguayo mwenyewe. paitwa au tuseme pajulikana kama kwa Mama Bonge... tutazidi kuwajuza menu zake zaidi kabla ya kukuelekeza alipo.

No comments:

Post a Comment