Monday, May 13

Viazi mviringo na rosti

   Kama kawaida ya mwisho wa wiki, kuna karatiba ka kutembelea ndugu, jamaa na marafiq, wikiendi hii, tulikatiza kwa mama Lulu na kuamua kulibariki jiko lake, kwa kuandaa viazi mviringo vikiwa na maganda yake pamoja na rosti ya mbuzi.
   Upishi wake ni rahisi sana, kwani wahitaji kuviosha viazi hadi viwe safi kabisa. Chukua sufuria safi yenye maji kidogo, kisha weka vipande vya viazi, chukua kitunguu maji, katakata kitunguu maji na weka pamoja na viazi, ongeza chumvi na weka jikoni vipate kuchemka kidogo, kama dakika 5 hivi.
   Hakikisha havichemki kabisa kwani vitapondeka, bali vinapata kulainika kidogo, kwani viazi hivi vitakaangwa kwenye mafuta. Epua viazi vyako, chuja kuondoa maji kisha weka kikaangio kwenye jiko, ongeza mafuta kisha acha yachemke na kaanga viazi vyako vikiwa na maganda yake.
   Muonekano unakua kama hivyo hapo kwenye picha

     Jaribisha upishi huu, unakua huchoki kula viazi vya mpiko mmoja, bali wabadilisha style. Ukishapika tutumie picha tuone vimetokelezeaje. Pembeni ni kikorombwezo cha kusindikizia menu hiyo.

No comments:

Post a Comment