Wednesday, March 20

Yatakayojiri 23.03.2013

   Muda tumekubaliana ni kuanzia saa 4 za asubuhi mpaka saa 10 za jioni, muda mzuri wa watoto kucheza, kula, kucheka, kuimba, kufurahi na watoto wenzao. Mfanya mwanao kuwa sababu ya mabadiliko kwa kumleta siku hiyo ya Toto day pande za Mbalamwezi, siku iliyotayarishwa na Menu Time wakishirikiana na K.A.B.L.E Inc, pamoja na Malaika Orphanage Foundation.
  Kiingilio ni shilingi za kitanzania 1,000/- kwa kila mtoto na shilingi 5,000/- kwa mtu mzima. Na kila sahani ya chakula ambapo kutakua na chipsi, sausage, kipande cha kuku na salad pamoja na juice itauzwa kwa shilingi 10,000/- tu.

  Iwapo utapenda mwanao avae fulana ambayo imetengenezwa maalum kwa shughuli hii, ina nembo ya Toto pamoja na ujumbe usemao Change inaanza na Mimi, basi tupe oda yako kupitia email yetu menutimes@gmail.com au kwa namba ya simu 0784 999 790, toa oda yako nasi tutakuletea.
  Karibuni sana Jumamosi pale Mbalamwezi Beach Club, mlete wenetu aweze kuwa sehemu ya mabadiliko.

No comments:

Post a Comment