Tuesday, March 19

Kuelekea Toto day 23.03.2013

   Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, tunaendelea kupata mawazo mengine mazuri, tukakaa tukafikiria na kuona ni vyema kama tutengeneza Tshirt za watoto zinazobeba ujumbe wa siku hiyo yaani Change inaanza na MiMi, kisha tuziuze kwa kiasi cha Tsh 10,000/- tu ambapo watoto wataweza kuzivaa siku ya Toto day pale Mbalamwezi beach Club.
   Tumesema kutakua na michezo, raha na furaha kwa watoto kuanzia saa 4 ya asubuhi mpaka saa 10 za jioni. karibuni sana wote kujumuika na watoto wa Malaika Orphanage Foundation pamoja na waandaaji ambao ni Menu Time na K.A.B.L.E Inc  
   Tshirt ina muonekano huu

   Rangi zilizopo ni Yellow, Nyeusi, Nyeupe, Brown, Kijani, Nyekundu na Kijivu ambapo zinapatikana katika size zifuatazo ambazo zinatosha kuvaliwa na watoto walio na umri wa miaka 3 -4, wa  miaka 5-6, wa miaka 7-8, wa miaka 9-11 na wa miaka 12 - 14. Iwapo mwanao yupo nje ya miaka iliyotajwa hapo tupatie size yake, nasi tutajitahidi kuhakikisha inapatikanika.
   Tupigie number hii 0784 999 790 kutoa oda yako, au tutumie email kupitia hapa menutimes@gmail.com. Karibuni sana!!

No comments:

Post a Comment