Thursday, March 21

Michezo itakayokuwepo siku ya Toto day

   Ni siku muhimu au maalumu kwa watoto wetu ambapo tunawakutanisha watoto kutoka majumbani na wale wa kituo cha Malaika Orphanage Foundation, wakutane wacheze, wafurahi, wale na mengineyo.
   Sasa tulivyosema kwamba tunataka wenetu wacheze vyema na wafurahi, tulihakikisha tunatafuta michezo ya watoto iliyo salama, ya kisasa na yenye ukubwa na nafasi ya watoto kujimwaya mwaya huku na kule.
   Kids Entertainment World ndio wadhamini wa upande wa michezo ya watoto. Na leo tunaona ushuhuda wa picha ambapo michezo hii itakuwepo kule Mbalamwezi Beach Club siku hiyo ya Jumamosi ya 23.03.2013.
   Karibu uone, mchezo huu waitwa Mary go round, yaani mwazunguruka humo ndani mpaka basiiiii

   Wa pili waitwa  The castle, mambo ya hekalu kama kwenye vijitabu vya story

   Kuna huu waitwa Noah's arc ambapo watoto wanacheza ndani humo huku wanakumbuka hadithi ya Noah

   Kana kwamba haitoshi, kuna mchezo huu wenye umbo la nyumba. Huu waitwa House!!

   Mchezo huu ni wa mwisho kwenye picha za leo ila sio kwamba ndio kwamba mingine haitakuwepo, laaah!! jina lililopewa ni Choochoo.

  Sasa ni wewe tu na uamuzi wako je, umlete mwanao au wanao waje kufurahi na wenzio au hutaki awe mmoja wa watakaoleta mabadiliko kwa kufurahi nasi?
   Jibu unalo. kiingilio ni shilingi 1,000/- kwa watoto na 5,000/- kwa wakubwa, pale Mbalamwezi Beach Club.

No comments:

Post a Comment