Tuesday, March 5

Tunaendelea na menu za mama Ruge

   Jana tuliona moja ya chakula cha asubuhi anachopata mama Ruge. Leo bado tupo kwenye kifungua kinywa, ila hapa ni tofauti kidogo ukilinganisha na kile tumeona jana. Hakuelezea ni wapi alipata menu hii, ila kwa picha tu yaonekana ilikua tamu sana.
  
   Kuna chai ya rangi yenye ndimu, mikate iliyookwa na kupakwa blue band, pamoja na maji ya matunda. Yaonekana ni nyepesi sana ikiwa na maana kuna zile siku hutaki kushiba sana asubuhi, basi mlo kama huo waweza kufaa nyakati za asubuhi.
    Asante sana muke ya muhaya, Mama Rige, Mage ambaye bado tupo nae kwa wiki hii nzima.

2 comments: