Friday, March 8

Menu za mwisho toka kwa mama Ruge.

   Tunamaliza wiki hii na kuendelea kuona menu anazozipata bibie Mage, ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Ruge a.k.a Ronny a.k.a Ronito, pia ni muke ya muhaya bwana Mashobe. Ukiondoa hayo ya nyumbani ni mwajiriwa ofisini kwake (hatupasemi), ni mfanyabiashara (mtafute kupitia sisi), ni Rafiq, ni Partner na dada yetu wa hapa Menu Time.
    Kuna menu mbili hapa..... Ya kwanza aliipata hapo alipokuwepo ambapo kuna samaki aliyemwagiwa rosti ya maana pia kuna chips pamoja na salad na mboga kwa pembeni.

 
    Ya pili ni take away, ambapo kuna viazi mviringo, nyama rosti na mboga mboga kwa pembeni..... hapa ni pale una njaa halafu upo kitaani na unapaswa kuwahi sehemu, basi unatoa oda take away na kusepa fastaaa.
     
Tunamshukuru sana, sana bi Mage kwa kuwa nasi wiki nzima bila ya kuchoka. Tunaamini ataendelea kutujuza mengi yahusuyo menu mara kwa mara. Iwapo nawe ungependa kushare nasi mapiko yako, menu unazokula n.k basi tutumie kupitia info@menutimetz.com au menutimes@gmail.com
    Asanteni sana na tunawatakia wikiendi njema na ya amani!!

2 comments:

  1. happy womens day muke ya muhaya na wadau wote wa menu time.hakika huyu ni mwanamke haswa.

    ReplyDelete
  2. Asante, indeed ni zaidi ya mwanamke, ni mama, mwajiriwa, Rafiq, shemeji, partners n.k

    ReplyDelete