Thursday, March 7

Kitaani na mama Ruge

   Tumeona vya asubuhi, tukaona mapishi yake..... yaani ile pilau tamu tuliyoona jana, na leo tunaona mama Ruge akienda kitaani na Rafiqs zake na mumewe mwenyewe, wanapata menu gani???? usiumize kichwa, kwasababu jibu tunalo hapa hapa. 
    Huu ni moja ya mlo ambao mamaaa Megvictor Mash kama wengi tunavyomuita hupendelea kuvipata haswaa tukiwa maeneo ya Shieni bar - Sinza, Hongera bar - Sinza, na kule Kigoma  kunapopatikanika menu hii.

   Hapo juu kuna ndizi tamu pamoja na kuku na vyote vimekaangwa vyema. Kwa mbali kuna vikorombwezo, wakina ndimu na chumvi na pilipili. 
   Suala la kuamua utashushia na nini, ni juu yako maana kwa mlo huo chochote kinaenda sawa, ni wewe tu!!
Endelea kumjua vyema mama Ruge kwenye upande wa menu kwa kutembelea humu humu menutime blog.

No comments:

Post a Comment