Friday, March 1

K.A.B.L.E & Menu Time ndani ya Malaika Orphanage Foundation

   Tunaendelea kukujuza yaliyojiri pale tulipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Orphanage Foundation kilichopo Kinondoni. Sasa basi.....baada ya kucheza sana michezo mbalimbali na kujuana. Tukaona turejee shuleni kidogo tukaamua kufundishana, kuchora, kupaka rangi na kujifunza matumizi ya kamera, kwa pamoja kama wanafamilia moja




   Kwa kweli tulipata raha na muda mzuri sana wa kucheza, kucheka, kufurahi, kujifunza, kupiga picha, kuwa karibu na wale wanaohitaji upendo zaidi, na kwa hilo tulisambaziana Upendo kati yetu. Ushuhuda wa furaha zetu ni huu


 



   Wakati yote hayo yanatendeka, kina dada walikua wanatayarisha maakuli, kwasababu moja ya ratiba zetu ilikua ni kupata chakula cha mchana na watoto wa Malaika. Na muda ulipowadia menu ilipakuliwa, iliandaliwa, ililiwa kwa pamoja na kushushiwa na maji ya matunda
   







   Tukasema tupige picha ya pamoja ya ukumbusho ili tuweze kukumbukana daima. Na hizi ni mojawapo ya picha tulizopiga


   Hakika ilikua ni siku ndefu yenye mafanikio mema, na kwa kujipongeza mkuu wa kituo alishushia na kinywaji baridi, huku akibadilishana mawazo na kinara wa msafara bwana Mutta


   Matukio yalichukuliwa kwa style mbalimbali, na wale waliokua wanachukua matukio pia walipata fiursa ya kupigwa picha wakiwa kazini. Kazi na dawa!!




   Kwa niaba ya K.A.B.L.E Inc, Menu Time inasema haya: "Tunashukuru Mungu, yote yalienda salama na kile tulichopanga kilifanikiwa. Tunawashukuru wote toka Malaika Orphanage Foundation kwa kukubali ombi letu la kuwatembelea kituoni, pia kutupa muda wao kukaa nasi. Tunashukuru kwa ukaribisho na shukrani zao kwa kidogo tulichopeleka. Tunaamini Umoja na Urafiq tulioujenga utadumu daima." Inshallah mpaka tutakaporejea tena Malaika Orphanage Foundation iliyopo Kinodonni, tumasema Cheers!!
   Kutoka Kituo cha Malaika kijulikanacho kama Malaika Orphanage Foundation, kilichopo Kinondoni, Menu Time imewahabarisha yaliyojiri siku ya Jumamosi 02.02.2013

No comments:

Post a Comment