Thursday, February 28

Tumerudi tena Arusha a.k.a A town

   Baba Ruge anaendelea kutujuza menu zilizopo pande za Arusha, zile anazokula yeye. Hapa alikuwa pande za Njiro, ilipo Nalopa Restaurant, huko Arusha, jiji lenye kila aina za raha. Kuanzia hali nzuri ya hewa, watu wazuri, pesa ya kumwaga, menu tamu na vimiminika navyo vyapatikana.
    Menu hiyo aliipata mida ya mchana na huu ndio ushuhuda wake

    Yaliyomo ni wali mweupe, nyama ya ng'ombe a.k.a fillet na salad pembeni ya kusindikizia menu nzima. Aina ya kimiminika cha kushushia menu hii ni chaguo lako mwenyewe maana mtoto wa Mashobe hakusema alishushia na kimiminika gani.
   Kutoka Menu Time tunasema Aikambe Chalii ya R!!

No comments:

Post a Comment