Friday, February 22

Menu Time ndani ya project ya K.A.B.L.E

   Tulisema mapema kwamba tuna mipango mingi zaidi ya kuongelea menu. Na moja ya mipango hiyo ni mpango wa kutoa misaada mbalimbali kadri ya uwezo wetu na jinsi ambavyo tutashirikiana na wenzetu. Sisi ni wanachama wa K.A.B.L.E ikimaanisha Keep Accessing Better Life Everyday. Tukatoa habari kwamba tunajipanga ili tuende kuwatembelea watoto yatima maeneo ya Kinondoni palipo Malaika Orphanage Foundation, ambapo kuna watoto kama 20 hivi wapo pale.
    Tulienda siku ya tarehe 2 ya mwezi huu wa pili, na tutakuja waletea habari zaidi ya yaliyojiri, yaani kituo kikoje, tulifanya nini na mipango ya mbele.
    Kukuonjesha ni picha ya wale walioandaa mpango mzima, wakiwa katika sare ya pamoja.


    Historia ya kila mwanachama yaani profile yao itakuja kwenu siku za usoni, kwa sasa tuwajue tu hata kwa majina. Kutoka pande ya kushoto ni Hakika, Fatna, Mutta, Tracy na Lulu. Tunawaletea stori kamili very soon.... Stay tuned!!

No comments:

Post a Comment